- 2,291 viewsDuration: 1:29Viongozi kutoka Kaunti ya Kilifi akiwemo Gavana Gideon Mung’aro wamewasuta Spika wa seneti Amason Kingi pamoja na mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini Aisha Jumwa Kwa kile walichokitaja kama njama ya kusambaratisha mpango wa serikali mseto. Viongozi hao wanadai licha ya rais William Ruto kuwataka viongozi kuheshimu makubaliano hayo, wawili hao wameonekana hadharani kupinga hatua hiyo. Viongozi hao waliyasema haya kwenye hafla ya kumteua Willis Okech kama kiongozi wa jamii ya Dholuo kaunti hiyo.