- 310 viewsDuration: 1:50Kuna haja kwa viongozi wa ngazi ya kaunti kuangazia zaidi ukuzaji wa talanta hasa kwa vijana chini ya umri wa miaka 16 kwani hatua hiyo itasaidia kuimarisha talanta zao. Hiyo ni kauli ya mwelekezi wa kiufundi wa FKF, Francis Kimanzi, akizungumza mjini Voi kaunti ya Taita Taveta wakati wa uzinduzi wa michuano ya Anderson Mtalaki. Aidha katika michuano hiyo timu zaidi ya 200 zitashiriki huku lengo ikiwa kukabiliana na dawa za kulevya hasa miongoni mwa vijana.