- 7,293 viewsDuration: 2:26Viongozi wa upinzani wakiongozwa na Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper, Rigathi Gachagua, Eugene Wamalwa na Justin Muturi wamelaani vikali ubomoaji uliofanyika katika eneo la Gikomba uliofanyika usiku wa kuamkia leo. Wakizungumza na wanahabari mjini Wote kaunti ya Makueni, viongozi hao walitaja tukio hilo kuwa la kinyama na lisilo na utu, wakimlaumu Rais William Ruto kwa kile walichodai ni dhuluma dhidi ya wananchi.