Skip to main content
Skip to main content

Viongozi walio mamlakani wahimizwa kusaidia kina mama Bungoma

  • | Citizen TV
    130 views
    Duration: 1:12
    Viongozi walio mamlakani katika kaunti ya Bungoma wametakiwa kujitokeza na kuwasaidia wananchi wa mapato ya chini katika jamii ili kujikimu kimaisha kwa kufadhili vikundi vya kina mama wanaondeleza miradi mbalimbali. Wito huo umetolewa na baadhi ya kina mama wa muungano wa malambisia women empowerment group katika Kijiji cha siboti eneo bunge la bumula baada ya kupokea shillingi millioni moja kutoka kwa mbunge wa kimilili Didmus Barasa pesa ambazo zitasaidia kuinua miradi ya maendeleo katika wadi hiyo. Kwa mujibu wa mbunge huyo kina mama ni nguzo muhimu katika jamii na hivyo ipo haja ya kuwapiga jeki ili kuboresha maisha kama njia moja ya kukidhi mahitaji yao na vilevile kukuza Uchumi.