Skip to main content
Skip to main content

Waasi wa M23 waingia Uvira, DRC. Je, hii itasambaratisha juhudi za amani?

  • | BBC Swahili
    21,777 views
    Duration: 7:50
    Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameingia katika mji wa mashariki mwa DRC wa Uvira, kituo muhimu cha jeshi la Congo karibu na mpaka na Burundi. Milio ya risasi na milipuko ya hapa na pale imeripotiwa wakati waasi hao wakiingia katika mji huo muhimu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, katika mashambulizi ambayo yamewalazimu maelfu ya watu kutoroka na kuvuka mpaka na kuingia Burundi. #DiraYaDuniaTV