Wabunge wameibua maswali kuhusu gharama ya ujenzi wa Bunge Towers

  • | Citizen TV
    360 views

    Wabunge wameibua maswali kuhusiana na gharama ya ujenzi wa jumba la ofisi za wabunge - Bunge Towers ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9.6, shilingi bilioni nne zaidi ya ilivyopangiwa. Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei ameitaka tume ya huduma za bunge -PSC - kuelezea vipi ujenzi wa jumba hilo umegharimu pesa nyingi ilhali jengo lenyewe sio la kisasa na baadhi ya miundombinu aidha haijakabilika au haifikii kiwango cha ubora. Cherargei amesema kuwa jumba hilo si salama huku akilalamika kuwa zaidi ya shilingi bilioni 1.5zimetumiwa kununua fanicha pekee.