Skip to main content
Skip to main content

WADAU WA UTALII NA MICHEZO KAUNTI YA KILIFI WAUNGANA ILI KUBORESHA SEKTA YA UTALII

  • | KNA Video
    83 views
    Duration: 2:35
    Sekta ya utalii mjini Malindi kaunti ya Kilifi inatarajiwa kuimarika hata zaidi kupitia michezo mbalimbali ambayo imeanzishwa katika eneo hilo hususan msimu huu wa likizo ya mwezi disemba. Kulingana na mkurugenzi wa bustani ya Buntwani mjini Malindi Ahmed Hassan hatua hiyo itavutia zaidi watalii wa ndani ya taifa la Kenya na wale wa kitaifa katika kutizama michezo hiyo. Akizungumza baada ya kutamatika kwa mchezo wa ufukweni uliohusisha mataifa ya Uganda, Tanzania na Kenya, mwenyekiti wa bodi ya manuspaa mjini Malindi Suleiman Salim amedokeza kuwa watatumia fursa hiyo ya michezo kuwatembeza wageni katika mbunga za wanyama kama njia mojawapo ya kutangaza maeneo hayo.