- 478 viewsDuration: 1:23Muungano wa hospitali za kibinafsi za mijini na mashinani umetangaza kusitisha matumizi ya bima ya afya ya umma ya SHA, na hivyo wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hizo watalazimika kujipilia bili zote. Kulingana na mwenyekiti wa muungano huo daktari Brian Lishenga, mfumo wa SHA umefeli kwani hospitali nyingi hazilipwi bili za matibabu chini ya bima hiyo.