Wagonjwa Wahamishwa Makadara Hospitali Kufanikisha Ubomoaji wa Jumba Mombasa

  • | K24 Video
    35 views

    Wagonjwa waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali Kuu ya Pwani, maarufu kama Makadara, wameanza kuhamishwa ili kutoa nafasi kwa ubomoaji wa jumba la ghorofa tisa lililoporomoka eneo la Kilifi Kona, Kaunti ya Mombasa. Zaidi ya wagonjwa 503 pamoja na wakazi wanaoishi karibu na eneo hilo wanahitajika kuhama, hasa wale walioko ndani ya eneo la kilomita moja mraba kutoka kwa jumba hilo. Ubomoaji huo utafanyika chini ya usimamizi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).