- 114 viewsDuration: 1:59Kwa siku 21, huduma za afya katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet zimelemazwa kutokana na mgomo unaoendelea wa madaktari. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyoibuliwa na madaktari hao, kama yalivyoainishwa katika mkataba wa kurejea kazini uliotiwa saini miaka miwili iliyopita, ni kupandishwa vyeo kwa madaktari, pamoja na kupangiwa kazi upya na kuongezewa malipo ya wale waliotafuata masomo zaidi.