Skip to main content
Skip to main content

Wahisani wasambaza sodo kwa wanafunzi Garissa

  • | Citizen TV
    294 views
    Duration: 1:53
    Idadi kubwa ya wasichana katika kaunti ya Garissa hukosa kuhudhuria masomo yao wakati wa siku zao za hedhi na hivyo kupata matokeo mabaya katika mitihani ya kitaifa. Takwimu kutoka kwa shirika la Together for Better zinaonyesha kuwa asilimia 86 ya wasichana katika kaunti hiyo hukosa masomo siku moja au zaidi wakati wa hedhi. Wahisani kama vile Benki la DTB pamoja na shirika Together for Better wameanzisha mpango wa kusambaza sodo kwa wasichana elfu saba katika kaunti nne za kaskazini mashariki ikiwemo Garissa.