Wanafunzi katika shule ya msingi ya Ruiru, kaunti ya Kiambu, wanayo sababu ya kutabasamu baada ya kupokea sodo takriban 3,000 kutoka kwa wasamaria wema, hatua inayolenga kuboresha usafi na kuhakikisha wasichana wanasalia shuleni bila vikwazo.
Kwa mujibu wa wadhamini, sodo hizo zimetengenezwa humu nchini na zinaweza kutumika mara nyingi hadi miaka mitatu iwapo zitatunzwa vyema, hivyo kupunguza gharama kwa wazazi na familia. Msaada huo unadhamiriwa kuziba pengo la wasichana wengi kukosa masomo au hata kuacha shule kwa sababu ya ukosefu wa sodo.