- 24,514 viewsDuration: 3:25Shughuli za kawaida zilitatizwa mapema leo mjini Kikuyu baada ya magenge ya wahuni kuwavamia watu. Biashara zilisalia kufungwa huku shughuli za usafiri pia zikiathirika, wenye magari wakihangaishwa na wahuni kwenye barabara ya Southern Bypass. Kilichoshangaza ni kuwa wahuni hao waliendelea na shughuli hizi mchana peupe bila wasiwasi wowote. Aidha, Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amewashutumu baadhi ya wanasiasa akisema ndio wahusika wakuu.