- 5,002 viewsDuration: 2:48Tukisalia kwenye kero ya wahuni, vijana waliojitokeza kujisajili kuwa wapiga kura chini ya mpango wa Niko Kadi walivamiwa na genge la wahuni walio vuruga kampeni yao mjini Kitale. Tukio hilo limeshutumiwa huku vijana wakiiitaka idara ya usalama kuwajibika na kutoa ulinzi wa kutosha kwenye hafla za kuhamasisha vijana kujitokeza ili kujisajili kama wapiga kura. Haya yanajiri huku IEBC ikitangaza kuwa wapiga kura wapya 875,501 wamesajiliwa tangu zoezi la usajili endelevu kuanza.