- 295 viewsDuration: 2:12Baadhi ya wakaazi wa maeneo ya Funzi na Msambweni katika kaunti ya Kwale wameweka makubaliano ya kuwekeza katika kilimo cha kisasa na ujenzi wa bandari kwenye mashamba yao. Wakaazi hao wameweka makubaliano hayo na kampuni ya Conkrite Capital kutoka Canada ambapo mapato ya kilimo hicho yatagawanywa baina ya wakaazi na mwekezaji. Uwekezaji huo unalenga ekari zaidi ya 64 kwa kilimo cha chai, matunda na mboga, mazao ambayo pia yatauzwa katika masoko ya nje ya nchi.