Wakazi Ongata Rongai wapinga kituo cha kujaza mitungi ya gesi

  • | KBC Video
    15 views

    Wakazi wa kijiji cha Nkaimurunya, eneo la Ong'ata Rongai kaunti ya Kajiado wameeleza wasiwasi kuhusu kituo cha kujazia mitungi ya gesi kilichoko katika maeneo ya makazi. Kwa mujibu wa ramani ya mipango y ujenzi ya kaunti, eneo ambapo kituo hicho kimejengwa limeratibiwa kuwa eneo la makazi wala sio kiwanda.Wakazi walioandaa mkutano wa kujadili suala hilo wanasema kituo hicho kilichoko katika kipande kidogo cha ardhi kimezungukwa na nyumba za makazi wakitaja hali hiyo kuwa inayohatarisha maisha yao. Wanaitaka halmashauri ya kudhibiti sekta ya kawi na asasi husika kuchunguza shughuli za kituo hicho na kuchukua hatua zifaazo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive