Skip to main content
Skip to main content

Wakazi Pioneer Estate wataka zoezi la ubomozi wa nyumba zao lisitishwe mara moja

  • | Citizen TV
    12,790 views
    Duration: 1:38
    Wakazi wa eneo la Pioneer Estate Barabara ya Outering Nairobi wametaka kusimamishwa mara moja kwa ubomoaji uliopangwa wa nyumba zao. Wanasema hatua hiyo ni ya ghafla na kinyume cha sheria, wakidai waliarifiwa tu kwamba ubomoaji huo unalenga kuwezesha mabadiliko ya njia ya bomba la maji taka. Wakazi hao wanasema taratibu hazikufuatwa ipasavyo, wakitaja ukosefu wa ilani, kutokuwepo kwa ushirikishwaji wa umma, na kutofanyika kwa mashauriano na wamiliki wa nyumba. Wanasisitiza kuwa nyumba zilizoathiriwa ziko kwenye ardhi inayomilikiwa kisheria na zina hati miliki halali za muda mrefu, hivyo si ardhi ya umma