Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Gatumbi walalamikia wizi wa vyuma vya daraja

  • | Citizen TV
    51 views
    Baadhi wa wakazi wa kijiji cha Gatumbi eneo la Gichugu Kaunti ya Kirinyaga wameendelea na maandamano ya kushinikiza kukamatwa kwa wahalifu wanaodaiwa kuiba vyuma vya daraja la Mto Nyamindi. Hii ni kufuatia ongezeko la visa vya wizi wa vyuma hivyo, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wanaotumia barabara za eneo hili. Wakazi wanasema kumekuwa na changamoto ya kuvuka mto huo haswa wakati huu ambapo Mvua inaendelea kunyesha katika eneo hilo, Wakazi wakitaka uchunguzi zaidi kuwakamata wanaohusika na uhalifu huo..