- 304 viewsDuration: 2:02Siku chache tu baada ya wakaazi wa Mariakani kaunti ya Kilifi kuandamana wakidai kutohusishwa katika ujenzi wa barabara eneo hilo sasa mamlaka ya kitaifa ya ujenzi wa barabara KENHA imeandaa kikao cha umma ili kuhamasisha utekelezaji wa mradi huo. Wakizungumza na wanahabari baada ya kikao hicho wakaazi wa Mariakani wamesisitiza umuhimu wa kuhusisha wananchi katika utekelezaji wa miradi mbali mbali pasi na wananchi kuandamana kwani ni haki yao ya kikatiba kupata taarifa kuhusu miradi inayotekelezwa.