Baadhi ya wakazi wa mji wa Nyamira wamelalamikia mrundiko wa taka mjini Nyamira, hali wanayosema imekuwa tishio kwa afya ya wakazi mjini humo.
Wakizungumza mjini Nyamira, wakazi hao wamelalamikia utepetevu wa serikali ya kaunti hiyo. Taka zimeziba aadhi ya maeneo na sehemu za barabara na kutatiza hata shughuli za uchukuzi. Aidha wakazi hao wanadai vijusi vinatupwa kwenye jalala. Wakazi hao sasa wametoa makataa kwa serikali ya kaunti na manispaa ya mji wa Nyamira kuchukua hatua za haraka kuzoa taka mjini humo la sivyo wakazi waandamane.