Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Sangin Elgeyo Marakwet washauriwa wahame vilima hatari

  • | Citizen TV
    697 views
    Duration: 1:53
    Wito umetolewa kwa wakazi wa kijiji cha Sangin, katika lokesheni ndogo ya Kokwao, kaunti ya Elgeyo Marakwet, kuhamia sehemu salama ili kuepuka majanga ya maporomoko ya ardhi . Haya yamejiri wakati ambapo hali ya hatari imeanza kudhihirika baada ya ardhi kuonekana kuanza kupasuka katika sehemu ya juu. Hali hii ikihatarisha maisha ya familia 11 zinazoishi sehemu za chini, hasa wakati huu ambapo mvua nyingi inaendelea kunyesha.