Wakazi wa Viragoni, wadi ya Mwanamwinga, eneo bunge la Kaloleni, kaunti ya Kilifi wanahofia kufurushwa baada ya ekari elfu tatu zilizoko ndani ya shamba la Kayafungo Group Ranch kutolewa hatimiliki chini ya serikali ya kaunti ya Kilifi kwa lengo la kutekeleza mradi wa kuinua eneo hilo kiuchumi .
Kulingana na wakazi hao hatua hiyo ni kinyume na makubaliano kati yao na serikali ya kaunti hiyo kwani awali walipimiwa mashamba yao na kuahidiwa kupewa hatimiliki ambazo hadi sasa hazijawafikia. Wakizungumza na wanahabari baada ya kikao cha kujadili mustakabali wa swala hilo wamekosoa serikali ya kilifi kwa kukiuka maagano .