- 120 viewsNi shilingi bilioni 1.4 tu ambazo hukopwa na kulipwa na wakenya kila mwezi katika hazina ya Hustler, licha ya hazina hiyo kupokea shilingi bilioni 14 kutoka Kwa wizara ya fedha. Haya ni Kwa mujibu afisa mkuu mtendaji wa hazina hiyo Henry Tonui ambaye anasema wameanza mikakati ya kuhakikisha waliokopa pesa hizo wanalipa. Hata hivyo wabunge wanachama wa kamati ya kuangazia hazina maalum wameibua tetesi kuwa kuna uwezekano kuwa zaidi ya shilingi bilioni 12 zimeporwa. Wabunge hao wakitaka stakabadhi zote kuhusu waliokopa kuwasilishwa Kwa kamati hiyo kubaini iwapo kweli pesa hizo zilikopwa au la.