Wakenya wahimizwa kukuza mianzi kwa ajili ya kukabiliana na baa la njaa

  • | K24 Video
    70 views

    Ili kukabiliana na uhaba wa chakula humu nchini, taasisi ya utafiti ya KEFRI inaendeleza mbinu ya kuzalisha mianzi kwa wingi ili itumike kama chakula mbadala. Sehemu inayoliwa ya mianzi huwa ni miche ambayo ina virutubisho muhimu na hupikwa kama chakula cha kawaida tu. kulingana na watafiti wa KEFRI kuna aina mbali mbali ya mianzi ambayo hukua kulingana na hali ya anga na hivyo kukumbatia mianzi kama chakula kutasaidia kukabiliana na baa la njaa.