Skip to main content
Skip to main content

Wakulima Sirisia walalamikia uhaba wa mbolea

  • | Citizen TV
    162 views
    Duration: 1:36
    Wakulima katika eneobunge la Sirisia kaunti ya Bungoma wamelalamikia uhaba mkubwa wa mbolea inayotumiwa baada ya upanzi, wakisema hali hiyo imeanza kuathiri shughuli za kilimo. Wakulima hao wanasema serikali imekuwa ikisambaza mbolea kwa kiwango cha chini katika ghala la mazao na nafaka la TAMLEGA ikilinganishwa na idadi kubwa ya Wakulima wanaotoka eneo hilo la Sirisia, Mlima Elgon, Kabuchai na hata kaunti jirani ya Busia. Wanasema wamekuwa wakipanga foleni ndefu Kwa zaidi ya siku tatu huku baadhi yao wakikesha usiku kucha wakisubiri mbolea. Hata hivyo afisa msimamizi wa ghala hilo Humphrey Mamai anasema uhaba huo umetokana na ongezeko la mahitaji ya mbolea .