- 9,519 viewsDuration: 41sMeli ya Villa Vie Odyssey ilianza safari ya kuzunguka dunia bila kikomo mwaka 2024. Hata hivyo, kampuni iliyokuwa ikiendesha safari hiyo iliishiwa na fedha. Kampuni hiyo ililaumu vita vya Iran kwa kupanda kwa gharama za mafuta. Baada ya kusimamisha shughuli, takribani abiria 200 walikwama nchini Kambodia. Tangu vita vya Iran vilipoanza mapema mwaka huu, bei za mafuta duniani zimepanda sana. Mwendeshaji wa meli hiyo alisema kuwa katika baadhi ya maeneo ya Asia, gharama ya mafuta kwa kila chumba kwa mwezi imepanda hadi dola za Marekani 8,000 (takribani pauni 6,000), kutoka dola 1,800. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw