Walemavu Tharaka Nithi wataka kutambuliwa na serikali

  • | Citizen TV
    234 views

    Kundi la walemavu katika eneo la Tharaka, Kaunti ya Tharaka Nithi linaomba viongozi kuwasambazia vyakula vya msaada. Kundi hilo linalalamikia makali ya njaa kufuatia kiangazi cha muda katika eneo hilo. Wanaoishi na ulemavu wamekuwa wakipitia masaibu ya kusajiliwa ili wafaidi hazina iliyotengewa walemavu. Wanawataka viongozi kufanikisha utoaji wa kadi za ulemavu ili waweze kutambulika. Watu hao pia wanaitaka serikali kuwajengea shule ya watoto wenye mahitaji maalum eneo la Tharaka kwani wanalazimika kuwapeleka watoto hao katika kaunti zingine.