- 908 viewsDuration: 1:48Chama cha UDA katika Kaunti ya Kwale kimeanzisha shughuli ya usajili wa wanachama mashinani ili kujiimarisha kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Shughuli hiyo iliongozwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho katika wadi ya Kubo South eneo la Shimba Hills waliowahimiza wakazi kujitokeza kwa wingi ili kujisajili kuwa wanachama wa UDA. wakazi zaidi ya 200 walisajiliwa katika kijiji cha Katangini .