Kamati ya bunge kuhusu nyumba imewataka wanakandarasi wanaotekeleza miradi ya nyumba za serikali kuhakikisha miradi hiyo inakamilishwa katika muda uliowekwa la sivyo watapokonywa kandarasi hizo..
Akizungumza mjini Hola wakati wa ukaguzi wa mradi huo, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mugambi Rindikiri amesema kuwa licha ya serikali kutoa pesa kwa wakati, wanakandarasi wengi wanajikokota kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kamati hiyo pia ilizuru eneo bunge la Garsen, na kusisistiza umuhimu wa wakandarasi kuwajibika ili kuhakikisha wananchi wananufaika na mradi huo wa kitaifa.