- 1,173 viewsDuration: 3:07Hali ya taharuki imetanda katika kijiji cha Chebtobot, eneo bunge la Marakwet Mashariki, baada ya wanakijiji wenye ghadhabu kuteketeza nyumba za familia kumi zinazodaiwa kuhusika na kifo cha kijana mmoja. Inasemekana kuwa Hosea Chemweno aliaga dunia akipokea matibabu mjini Eldoret baada ya kuvamiwa na vijana watatu wa familia jirani. Wakazi wanadai kwamba mara kwa mara vijana hao hukamatwa na kuachiliwa baadaye.mahakama.