- 223 viewsDuration: 1:51Matumizi mabaya ya mtandao na utapeli ni baadhi ya changamoto kubwa zinazoshuhudiwa na wakaazi wa kaunti ya Garissa na sasa kanuni za kuthibiti utoaji wa huduma mitandaoni zianzishwe. Kwenye vikao vya kutoa maoni, wizara ya hazina ya kitaifa imekusanya maoni kote nchini yatakayotoa mwongozo wa namna watoaji huduma za kidijitali watakavyofanya kazi humu nchini na vile vile kuunda sheria za kulinda wananchi dhidi ya matapeli. Maafisa kutoka wizara hiyo wamehakikishia wakazi kuwa maoni yao yatajumuishwa wakati wa kuunda sheria ili kuwaondolea wasiwasi.