- 1,058 viewsDuration: 4:03Wanawake kutoka wadi ya Magadi, Kaunti ya Kajiado wameapa kutoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 Iwapo serikali haitajitokeza na kuruhusu uchaguzi wa muungano wa wanawake katika eneo hilo. Wakizungumza baada ya kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi ambao kwa mara Nyingine tena uliahirishwa, wanawake hao wanasema uchaguzi wa viongozi wa wanawake umejikokota kwa zaidi ya miaka 28 na kuwanyima wanawake sauti za kujitetea ikizingatiwa kuwa wanawake wanapitia changamoto nyingi huko Magadi.