Skip to main content
Skip to main content

Wapatanishi wa Marekani, Urusi na Ukraine kukutana. Watafanikiwa kumaliza vita?

  • | BBC Swahili
    3,374 views
    Duration: 3:49
    Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine amesema yuko katika hatua muhimu ya kumaliza vita na Urusi, akielezea kikao kinachotarajiwa kufanyika cha wajumbe wa mataifa ya Ukraine, Urusi na wapatanishi kutoka Marekani katika mji wa ABU-DHABI, katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE kwamba huenda ukawa ni wa matumaini. Hii ndio mara ya kwanza kwa wajumbe wa mataifa hayo matatu kufanya kikao cha pamoja tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake ndani ya UKraine miaka minne iliyopita. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw