Skip to main content
Skip to main content

Waporaji wanaswa kwenye kamera wakivamia duka la vito

  • | BBC Swahili
    4,780 views
    Duration: 31s
    Kamera za CCTV zanasa tukio la vibaka wakivamia duka la vito nchini Ufaransa Duka hili la vito lilivunjwa na kuvamiwa mjini Lyon, Ufaransa, wakati maandamano yanayoongozwa na wanafunzi yakiendelea baadhi ya watu wanatumia fursa hiyo kufanya uporaji. Kamera za CCTV zilionyesha wakivunja madirisha ya duka la vito la Koumal kabla ya kupekua droo, kufanya uharibifu na kuiba vitu mbalimbali. Shirikisho la Biashara na Uuzaji wa Rejareja limesema karibu maduka 3,000 yameathiriwa nchini kote mwishoni mwa wiki, huku serikali ikikosolewa kwa kushindwa kudhibiti usalama. #bbcswahili #ufaransa #maandamanoufaransa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw