WASHINGTON BUREAU-TRUMP AKUTWA NA HATIA YA UNYANYASAJI WA KINGONO KATIKA MAHAKAMA YA NEW YORK

  • | VOA Swahili
    704 views
    Jopo la mahakama la serikali kuu mjini New York, Jumanne lilimpata na hatia rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ya kumyanyasa kingono mwanake mmoja, na kutoa kauli za uongo kumhusu. Mahakama imemuamuru Trump amlipe mlalamishi, Jean Caroll, dola milioni tano, milioni mbili kwa kumnyanayasa kingono, na milioni tatu kwa sababu ya kutoa habari za uongo kumhusu. Trump amendelea kusisitiza kuwa hakumfahamu mlalamishi, na kwamba tuhuma hizo ni za uongo na zilizochochewa kisiasa. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.