- 188 viewsDuration: 3:11Wataalamu wa afya wanawataka wakulima kote nchini kuwekeza katika kilimo cha mboga za kiasili ili kujipatia mapato ya haraka pamoja na kuimarisha afya ya jamii kutokana na uwepo wa madini muhimu yanayopatikana katika mboga hizo. Wanasema mboga za kienyeji zina uwezo mkubwa wa kusaidia kupunguza utapiamlo na magonjwa yanayotokana na lishe duni.