- 1,038 viewsDuration: 1:32Shirika la kutetea haki za binadamu la Centre For Litigation Trust limetishia kuelekea mahakamani kuishinikiza serikali kulipa fidia na kuhakikisha miili ya wakenya waliofariki nchini Urusi imerudishwa nchini. Wakizungumza huko Mtwapa kaunti ya Kilifi wameilaumu serikali wakisema ziara ya mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi nchini Urusi ilipaswa kushughulikia jinsi familia za waathiriwa zitawapata wapendwa wao au miili ya jamaa zao. Katika kikao hicho wametaka serikali kukabiliana na ongezeko la visa vya mauwaji na utekaji nyara nchini.