Watoto hamsini wamepokea ufadhili wa miguu bandia Kajiado

  • | K24 Video
    92 views

    Jamii ya wanaoishi na ulemavu hasa wasio na uwezo wa kutembea kwa ukosefu wa miguu hupitia changamoto tele kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine. Hata hivyo ilikua ni afueni kwa zaidi ya watoto 50 waishio na ulemavu wa miguu na mikono kutoka sehemu tofauti nchini baada ya wahisani kuwafaa kwa kuwapa vifaa vya kutembea katika hafla ya kufana katika hospitali ya AIC CURE International, ambapo walionufaika walitembea kwa madaha juu ya zulia jekundu huku wakishangiliwa.