- 870 viewsDuration: 1:56Watu 10 wamedhibitishwa kufariki huku 6 zaidi wakiuguza majeraha mabaya baada ya ajali katika eneo la Kodada kaunti ndogo ya Rachuonyo East katika kaunti ya Homa Bay. 10 hao wameripotiwa kufariki Jumapili usiku waliokuwa safarini kurudi nyumbani kutoka Kakamega walipohudhuria hafla ya harusi, kabla gari hilo kupata ajali pamoja na malori mawili katika barabara kuu ya kutoka Kisumu kwenda Kisii. Sita waliojeruhiwa walihudumiwa katika hospitali ya Rachuonyo South mjini Oyugis kabla kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Nyamira kwa matibabu zaidi.