- 7,323 viewsDuration: 51sWatu sita wameaga dunia kwenye ajali mbili tofauti katika kaunti za Nakuru na Makueni. Watu wanne walifariki baada ya trela mbili kugongana ana kwa ana katika eneo la Kiunduani Makueni, kwenye barabara ya Mombasa - Nairobi. Ajali hiyo ilisababisha moto mkubwa ulioteketeza magari yote mawili. Wanne walioaga ni madereva wawili, mwanamke na mtoto wake ambao walikuwa wameabiri gari moja. Na katika eneo la Soysambu, Gilgil, kaunti ya Nakuru watu wawili wameaga dunia baada ya gari la kibinafsi walimokuwa kugongana na trela lililokuwa likielekea upande wa Nakuru.