- 9,836 viewsDuration: 2:18Watu waliojihami kwa bunduki waliwavamia na kuwauwa watu wanane, wakiwemo wahandisi watano, maafisa wawili wa akiba na dereva, katika eneo la Hagarsu, kwenye barabara kuu ya Mandera-Arabia-Lafey, kaunti ya Mandera. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti hiyo, Robinson Ndiwa, washambulizi walivizia gari lililokuwa limewabeba wafanyikazi hao wa barabara waliokuwa wakilindwa na maafisa wa NPR na kulimiminia risasi. Na kama anavyoarifu Feisal Abdirahman, wakazi wanasema wavamizi hao walifunga barabara kabla ya kulimiminia gari hilo risasi.