- 2,016 viewsDuration: 1:57Watu wawili ikiwemo raia wa Tanzania wamekamatwa katika mpaka wa Namanga, Kaunti ya Kajiado baada ya kupatikana na pembe za ndovu zenye uzito wa kilo 110, ambazo thamani yake inakadiriwa kuwa shilingi milioni 11. Washukiwa hao Imani Manasi Msumbwa mwenye umri wa miaka 28 na Alton Jilaoneka Kenga mwenye umri wa miaka 33 walikamatwa kufuatia taarifa za kijasusi kutoka kwa wenyeji. Inadaiwa washukiwa hao walikuwa wakisafirisha pembe hizo kutoka Malawi kwa kutumia gari aina ya Toyota Mark X. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive