Wauguzi na mataalamu wa maabara katika Kaunti ya Laikipia wameandamana katika mji wa Nanyuki huku mgomo wao ukiingia siku ya nne.
walianza maandamano yao katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Nanyuki na kupita katikati ya mji hadi ofisi ya Gavana, ambako walidai kukutana na maafisa wa kaunti. Huku wakiwa wamebeba mabango, wahudumu hao wa afya waliapa kuendeleza mgomo huo hadi malalamishi yao yote yashughulikiwe kikamilifu. Miongoni mwa matakwa yao ni utekelezaji kamili wa makubaliano ya kurejea kazini .