Skip to main content
Skip to main content

Waumini na viongozi wa ELCK waendeleza mzozo wa miaka unatokana na kuwepo kwa maaskofu wawili kanisa

  • | Citizen TV
    374 views
    Duration: 2:13
    Mzozo wa uongozi unaendelea kutokota katika kanisa la ELCK jimbo la Nyamira, makundi mawili yaking'ang'ania uongozi wa jimbo la kanisa hilo baada ya kuidhinishwa kwa maaskofu wawili mwaka jana. Mrengo mmoja umemnyoshea kidole cha lawama askofu mkuu wa kanisa hilo nchini Dkt. Joseph Ochola, kwa madai ya usimamizi mbaya wa rasilimali za kanisa na matumizi ya katiba isiyo halali inayokandamiza baadhi ya viongozi wa kanisa hilo. Wakizungumza na wanahabari mjini Nyamira, viongozi hao wamemshauri Askofu Mkuu Joseph Ochola kuunganisha kanisa hilo na kutumia sheria na katiba halali.