- 592 viewsDuration: 3:11Muungano wauzaji mafuta wadogo wanakiri kuwepo kwa uhaba wa mafuta wanaodai kuwa unachangiwa na kampuni kubwa za mafuta kukataa kuwauzia bidhaa hiyo. Wauzaji mafuta hao sasa wanaitaka serikali kufutiliwa mbali mkataba wa mafuta kati ya Kenya na mataifa ya Uarabuni wakisema kuwa wananunua mafuta kwa bei ghali na kuhitajika kuuza bidhaa hiyo kwa hasara. Meli za mafuta zinawasili katika bandari ya Mombasa kuashiria kuwa huenda uhaba ukakosa kuonekana katika siku za karibuni.