- 270 viewsDuration: 1:16Migogoro ya kijamii katika kaunti ya Tana River imechangia kaunti hiyo kukosa wawekezaji. Akizungumza wakati wa kukabidhi kampuni ya moja kutoka Canada barua ya mgao wa kipande cha ardhi, Gavana wa kaunti hiyo Dhadho Godhana amesema siasa za chuki na uchochezi zimerudisha nyuma kaunti hiyo kimaendeleo. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga nyumba elfu kumi kupitia mpango wa uwezeshaji na kutoa nafasi za biashara za kijamii hasa kwa waathiriwa wa mafuriko.