Wazee kutoka jamii ya Waluhya wawahimiza vijana kuhubiri amani na kutafuta vitambulisho

  • | Citizen TV
    355 views

    Wazee kutoka jamii ya Waluhya wanawahimiza vijana kuhubiri amani na kutafuta vitambulisho ili kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao na kuwachagua viongozi bora.Aidha, wazee hao kutetea umoja wa Wakenya ili kupunguza joto la kisiasa linaloshuhudiwa katika taifa hili. Wamewasuta baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kutumia lugha ya chuki ili kujipatia umaarufu, na kuwataka kuwa kielelezo kwa jamii.