- 287 viewsDuration: 2:09Baraza la wazee kutoka jamii ya Luhya wamekutana kuweka mikakati ya kukabiliana na kauli kali kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, ambazo wanasema zinaweza kuhatarisha mshikamano na amani katika jamii. Wakizungumza mjini Kitale, wazee hao wamesema wameanzisha mipango ya kuwaita viongozi kutoka jamii yao ili kuwapa mwelekeo kuhusu umuhimu wa siasa za amani, huku wakisisitiza kuwa viongozi wana wajibu wa kuhubiri umoja badala ya chuki.