Waziri Owalo aongoza mahafali Chuoni KIMC

  • | KBC Video
    21 views

    Vijana wametolewa changamoto ya kujinufaisha kupitia nyanja ya kidijitali kutokana na uwekezaji unaoendelezwa na serikali. Huu ulikuwa wito wakati wa mahafali ya kuhitimu kwa wanafunzi katika taasisi ya mawasiliano nchini KIMC katika mtaa wa South B, Nairobi. Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi wa kidijitali Eliud Owalo alitoa changamoto kwa wanafunzi waliohitimu kukumbatia fursa zinazopatikana katika nyanja ya teknolojia ili kubuni maudhui na vilevile kudumisha uadilifu wa uandishi wa habari na kubainisha ukweli kabla ya kuchapisha taarifa. Wakati wa hafla hiyo, watahiniwa 457 walikabidhiwa vyeti vya Diploma na vyeti vya taaluma mbalimbali.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News