Skip to main content
Skip to main content

Waziri Ruku azungumzia polisi wanaofanya kazi ya udereva

  • | Citizen TV
    700 views
    Duration: 2:04
    Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku ameitaka tume ya huduma kwa umma kuhakikisha kuwa maafisa wa polisi waliopewa kazi za udereva katika mashirika mbalimbali ya serikali wanaruhusiwa kurejea kwenye majukumu yao ya msingi ya kulinda usalama na kudumisha sheria. Akizungumza katika eneo la Kaplamai, Ruku amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya maafisa wa polisi wakitumiwa kama madereva katika taasisi za serikali ilhali taasisi hizo zina madereva wao wanaolipwa na serikali. Alieleza kuwa hali hiyo imechangia upungufu wa maafisa wa polisi wanaotekeleza majukumu ya usalama, akisisitiza kuwa ni muhimu kila afisa arejeshwe katika jukumu lake. Aidha, aliitaka Tume ya Utumishi wa Umma kushirikiana na wizara husika ili kuhakikisha kuwa mpangilio sahihi wa rasilimali watu unazingatiwa katika taasisi zote za serikali.